Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WATUMISHI SEKTA YA AFYA WASISITIZWA MAHUSIANO MAZURI KAZINI ILI KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Posted on: February 8th, 2024

Na WAF, Rukwa

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amewasisitiza watumishi katika Sekta ya Afya nchini kudumisha Mawasiliano baina yao na wagonjwa ili kujenga mahusiano mazuri baina ya mtumishi na Mgonjwa au ndugu wa mgonjwa.


Ameyasema hayo leo tarehe 8 Februari, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Rukwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga iliyolenga kukakua usimamizi wa utendaji kazi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya .

 

Dkt. Magembe amesema wagonjwa ni vyema kumfanya ajisikie yuko sehemu salama kwa kumpa maelezo juu ya mazingira ya Hospital ni wajibu wa mtoa huduma kumpatia mwelekeo ya kufahamu Mazingira hayo.


“Mgonjwa anapofika hospital au kituo cha afya chakufanya kwa mtoa huduma ni kujitambulisha na muelekeza wa vyumba vya madaktari vilipo, wodi na vyoo hii itamfanya mgonjwa kuwa huru na kutengeneza mahusiano mazuri baina yako na mgonjwa na utamfanya ajisikie yuko sehemu salama, na ndio maana halisi ya huduma bora kwa mteja” 


Dkt. Magembe Ameongeza kuwa ni lazima katika kila hospital na vituo vya kutolea huduma za Afya nchini kupandika namba za mawasiliano ili mwananchi anapopata changamoto iwe Rahisi kupata msaada.


“Maelekezo yalishatolewa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Makatibu Wakuu na hata Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kuwa katika kila eneo la huduma lazima tubandike namba zetu za simu ili Kama mgonjwa au ndugu wanahitaji maelekezo, kutoa pongezi au kakutana na changamoto ni Rahisi kutoa taarifa yake na kupata msaada “ Amesema Dkt. Magembe 


Aidha Dkt. Magembe amesisitia kuwa Mtoa huduma kumpatia taarifa mgonjwa juu ya ugonjwa unaomsumbua na sio kumuacha aondoke bila kujua kinachomsumbua.


“Nisisitize kwenye suala la huduma kwa mteja, unapomfanyia uchunguzi mgonjwa na ukagundua tatizo lake basi mwambie ugonjwa unaomsumbua na hata dawa ulizompa mwambie zitamsaidia kitu gani” amesema.