Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERIKALI, KOFIH KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI MAGONJWA YA MLIPUKO

Posted on: February 19th, 2026

Na Clement Robert, WAF – Dar es Salaam


Wizara ya afya kupitia maabara ya taifa ngazi ya jamii imefanya mapitio ya mradi wa kazi za mwaka wa tatu na shirika la Korea KOFIH wenye lengo la kuijengea uwezo maabara ya taifa ili kutambua magonjwa ya mlipuko 


Hayo yamebainishwa leo Februari 19, 2026 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa maabara ya taifa ya afya ya jamii Bw. Ambele Mwafulango wakati wa uzinduzi wa mradi wa kazi za mwaka wa tatu naina ya Korea na maabara ya taifa 


Amesema asilimia kubwa ya mambo yalipangwa ndani ya miaka miwili kwenye mradi huo wa miaka mitano yametekelezwa ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vya maabara, vitendanishi na kujengea uwezo maabara ya taifa juu ya utambuzi wa magonjwa ya mlipuko


“Kwa tathmini tuliyoifanya, utekelezaji wa mradi umefikia hatua ya kuridhisha ndani ya miaka miwili ya mwanzo. Tumeimarisha miundombinu ya maabara, tumepata vifaa na vitendanishi vya kisasa, pamoja na kuongeza ujuzi kwa wataalamu wetu ili kuweza kubaini kwa haraka na usahihi magonjwa ya mlipuko,” amesema Bw. Mwafulango.


Bw. Mwafulango amesema zaidi ya milioni 694 zitatumika wakati wa kutimiza malengo ya mradi huo kwa mwaka wa tatu unaoanza, huku kwa mwaka wa kwanza ukitumiza zaidi ya Milioni 400 na mwaka wa pili ikiwa ni Milioni 674


Naye Dr. Hanson Park kutoka Shirika la Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) amesema mradi huo unalenga kuimarisha mifumo ya uchunguzi na ufuatiliaji wa magonjwa kama dengue, kipindupindu na magonjwa mapya ya mfumo wa upumuaji, kwa kutumia teknolojia za kisasa ikiwemo NGS.


“Kuna umuhimu wa wadau wote kuzingatia miongozo ya utekelezaji wa mradi pamoja na kuwasilisha mapendekezo ya shughuli za miaka ijayo kwa ajili ya upangaji madhubuti na hata huu ushirikiano na uwajibikaji ni msingi wa mafanikio ya mradi huu tukiazimia kwa pamoja


Aidha Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Kinga Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle amesema wanahakikisha wananchi wanapata elimu ya kujikinga na maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza kupitia waratibu wa sehemu ya elimu ya afya kwa umma pamoja na kaguzi mbalimbali za maeneo yenye viashiria vya magonjwa mbalimbali