Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WATAALAM KADA ZA AFYA WAFUNDISHWE KUENDANA NA MAHITAJI YA NYAKATI

Posted on: July 17th, 2024

Na WAF - KIGOMA


Katika kuendelea kuimarisha ubora wa huduma za Afya nchini, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amewataka wakufunzi wa vyuo vya Afya nchini kuhakikisha wanafundisha wanafunzi wa kada hiyo kufuatana na mabadiliko ya teknolojia na wakati ili waweze kuleta tija zaidi katika maendeleo ya sekta ya Afya kwa siku za usoni


Mganga Mkuu amesema hayo Julai 16, 3024 mkoani Kigoma wakati alipotembelea kituo cha mafunzo ya maafisa wa kliniki na chuo cha mafunzo cha Kigoma Training College ambapo amesema Sekta ya Afya ni miongoni mwa sekta zenye mabadiliko ya kila siku hivyo ni vyema wanataaluma hao kuhakikisha wanakuja na taaluma ambazo zinakwenda na wakati na wanafunzi waweze kutoka na ujuzi wa kutosha


Pof. Nagu amesema katika kulifanikisha hilo iko haja ya kuanza kwa kuwapa mafunzo, taaluma na ujuzi mpya mara kwa mara walimu wanaofundisha wataalamu hao. 


“Walimu wanaofundisha hawa wataalamu wetu wapewe mafunzo kwa kuendana na mabadiliko ya wakati na pia wawe macho kuona mabadiliko na kutushauri tuongeze nini wapi ili hawa wataalamu watakao wapika waweze kuwa na tija kwa kuendana, kulingana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na nyakati“ Amesema Prof. Nagu


Pia ameviasa vyuo vya Afya kuisaidia serikali kushughulikia uhaba wa wataalam kwa baadhi ya taaluma katika sekta hiyo hususani kwa kuja program zinaendana na mahitaji ya jamii.


“Hatuna wataalamu wa Radiolojia, wale wanaofundisha usikivu, tuna uhaba mkubwa wa wataalamu wa maabara, kwahiyo sekta hizi naomba mziangalie na pengine wala haziitaji miundombinu mikubwa sana, tusaidiane kuhakikisha wataalamu hawa.” Amesema Prof. Nagu



Prof. Nagu amesisitiza walimu kada za Afya pia kuhakikisha suala la maadili na nidhamu za watoa huduma linaimarika tangu vyuoni kwani ni nyenzo muhimu katika kuimarisha ubora wa huduma za Afya nchini.



Mganga Mkuu wa Serikali pia amepata fursa ya kutembelea vyuo vitakavyokuwa vinafundisha wataalam wa afya ngazi ya jamii, katika vyuo viwili vya Kituo cha Mafunzo ya Maafisa wa Kliniki (Kigoma COTC) na kigoma Training College kuridhika na Maandalizi