Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WANANCHI SHINYANGA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA

Posted on: October 17th, 2025

Na WAF - Shinyanga

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga, Jakaya Kikwete, Dkt. Charles Mlonganile, amesema ujio wa madaktari bingwa umepokelewa kwa mwitikio mkubwa na wananchi wa wilaya hiyo, kwani ndani ya siku mbili za mwanzo watu zaidi ya 250 wamejitokeza kupata matibabu ya kibingwa hospitalini hapo.

Akizungumza Oktoba 17, 2025, mkoani Shinyanga wakati wa kambi ya Madkatari Bingwa wa Rais Samia, Dkt. Mlonganile amesema ujio wa madaktari hao umeleta manufaa makubwa kwa wananchi kwani umewarahisishia upatikanaji wa huduma za kibingwa na bobezi kwa urahisi zaidi.

Dkt. Mlonganile amesema mpango huo umewawezesha madaktari wa ndani kuongeza ujuzi kwa kujifunza mbinu mbalimbali za utoaji huduma kwa wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.

Aidha, Dkt. Mlonganile ameishukuru Serikali kwa kusogeza huduma za kibingwa na bobezi karibu na wananchi wa mkoa wa Shinyanga kupitia hospitali ya Jakaya Kikwete, akisema hatua hiyo imepunguza gharama na changamoto walizokuwa wanakutana nazo wananchi walipolazimika kusafiri mbali kufuata huduma hizo.