Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

UJUMBE WA RAIS SAMIA UMEPOKELEWA NA MHESHIMIWA YUSUF MAITAMA TUGGAR WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NIGERIA.

Posted on: July 13th, 2024

Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya na Mjumbe Maalum wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Julai 13, 2024 amewasilisha ujumbe maalum kwa Mhe. Bola Ahmed Tinubu, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Nigeria.


Ujumbe wa Rais Samia umepokelewa na Mheshimiwa Yusuf Maitama Tuggar Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria.


Mheshimiwa Tuggar baada ya kupokea ujumbe huo maalum kwa niaba ya Rais Tinubu amesema kuwa atamfikishia ujumbe huo maalum Mheshimiwa Rais na amezipongeza nchi mbili hizi kwa ushirikiano wa undugu uliodumu kwa muda mrefu tangu enzi za Waasisi wa Mataifa haya mawili na hususani wakati wa kupigania uhuru enzi za uongozi wa Hayati Babati wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Namdi Azikiwe, Rais wa Kwanza wa Nigeria.


Kwa upande wake Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Serikali ya Nigeria kwa mapokezi mazuri ya timu ya ujumbe maalum wa Dkt. Samia na ameahidi kuendeleza mashirikiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili katika Sekta mbalimbali ikiwemo Afya na Elimu.