TUMIENI MAJUKWAA YA MICHEZO KUIMARISHA AFYA
Posted on: July 28th, 2024
Na WAF - Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Afya kuendelea kushirikiana na wadau wanaoandaa michezo ya riadha na mengineyo kwa lengo la kutumia majukwaa hayo kufikisha elimu ya afya kwa umma na kubali mitindo ya maisha inayochochea ongezeko la Magonjwa yasiyoambukiza.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito huo Julai 28, 2024 wakati akihitimisha mbio za NBC Marathon iliyokuwa na lengo lakuchangia huduma za afya pamoja na kuimarisha afya kwa njia ya mazoezi.
“Wizara ya Afya endeleeni kushirikiana na wadau wote wa michezo wanaondaa michezo hii inayotuleta wote kwa pamoja kwa lengo lakufikisha elimu ya umuhimu wa kufanya mazoezi kama ambavyo leo tulivyofanya" Amesema Majaliwa
Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa mbali mbali Wizara ya Afya zinaonyesha kwa siku za karibuni Magonjwa yasiyo ambukiza yameongezeka tofauti na hali ilivyokuwa huko nyuma na hususani ni Magonjwa ya kisukari, sinikizo la damu, Moyo na Figo.
“Kwenye eneo hili ni muhimu tuendelee kupokea ushauri wa wataalam wa afya, kukaa bwete ni kukaribisha magonjwa hayo yasiyoambukizwa ni muhimu kushiriki katika michezo mbalimbali na mimi naamini sote tumeanza kujali kwa kuzingatia kufanya Mazoezi” amesema Waziri Mkuu Majaliwa
Waziri Mkuu ametumia wasaa huo kuishukuru Benki ys NBC kwa niaba ya watanzania kwa kuendelea kushirikina na Serikali kuchangia na kuwezesha uboreshaji wa sekta ya Afya kwa maeneo yanayogusa Ustawi wa jamii.
“Mbio hizi zimekusanya michango mbalimbali kwa lengo la kuisaidia Sekta ya Afya, NBC mmendelea kutuonyesha njia kwa ubunigu wenu wa kukusanya Fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye Sekta ya Afya, Fedha ambayo ameitaja Mkurugenzi Mkuu Millioni 300 ambayo itakabidhiwa leo ni kwa lengo ya kuusaidia mapambano dhidi ya Kansa ya Mlango wa shingo ya kizazi kwa wanawake ambayo itakabidhiwa kwa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road,