Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SIKU TATU WAGONJWA ZAIDI YA 300 SIKONGE, KAMBI YA MADAKTARI BINGWA

Posted on: June 12th, 2024


Na WAF, SIKONGE, TABORA


Wananchi zaidi ya miatatu wilayani Sikonge mkoani Tabora, wamejitokeza ili kupata huduma za kibingwa zinazotolewa na Madaktari Bingwa wa Mama Samia.


Hali hiyo imebainishwa Juni 12, 2024 na Dkt. Richard Sindani Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo Kikubwa cha Afya cha Mazinge kinachofanya kazi kama Hospitali ya Wilaya.


Dkt. Sindani amesema katika kipindi cha Siku tatu miongoni mwa wananchi 300 waliojitokeza, kumi kati yao walifanyiwa huduma za upasuaji


“Kati ya hao kumi, watatu hawa kama sio ujio wa Madaktari Bingwa tungelazimika kuwapa rufaa kwenda Kitete Hospitali ya mkoa kwa huduma za kibigwa” amefafanua Sindani.


Akizungumza kwenye Mahojiano Maalum Dkt. Husmond Diegula Daktari Bingwa wa upasuaji wamefanikiwa kupata wagonjwa kumi na tano waliohitaji upasuaji


“Tulimpata mama ambaye alikuwa na Mawe kwenye Nyongo, huyu tumepanga kumfanyia upasuaji siku ya leo” amesema Diegulla


Kwa upande wao wananchi waliofika kupata huduma wameiomba Serikali kufanya huduma hiyo kuwa endelevu na matangazo yatolewe vyakutosha


Bibi. Grace Chambi na Jane Sungura wakaazi wa Sikonge, wamesema waliposikia kupitia TV ujio wa Madaktari Bingwa waliamua kuchukua hatua


“Sio kila mtu anauwezo wakwenda Kitete au Bugando, hivyo tunazidi kumuomba Mama Samia hii huduma iwe endelevu” amesema Bi. Chambi.


Kwa upande wake Bi Sungura yeye amesema, Rais Samia ametambua shida za wamama na changamoto zao kwakuwa na yeye ni Mama, tunamuombea azidi kutukumbuka hata marabili au tatu kwa mwaka.


MWISHO