MADAKTARI BINGWA WA DKT. WATAKIWA KUENDELEA KUWA CHACHU YA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA
Posted on: May 19th, 2025
Na WAF, Rukwa
Timu ya Madaktari Bingwa thelasini na watattu.
(33) wa Rais Dkt. Samia wameaswa kujikita kuleta suluhu ya changamoto za kiafya zinazozikumba hospitali za halmashauri na Kuhakikisha wanaendelea kuwa chachu ya mapinduzi ili kuboresha huduma za afya ngazi ya msingi.
Rai hiyo imetolewa Mei 19, 2025 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Bw. Msalika Makungu Wakati wa zoezi la Mapokezi ya Madaktari Bingwa Mkoani Rukwa ambapo
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Bw. Msalika Makungu amesema kuwa, ujio wa Madaktari Bingwa hao unalenga kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi, ili kuimarisha huduma za mama na mtoto na huduma nyingine za kibjngwa ikiwa sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya waliopo kwenye vituo vya afya na hospitali za Wilaya.
Amempongz Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuleta huduma za kibingwa mara kwa mara mkoani hapo.
"Huduma zitakazotolewa na madaktari bingwa hao ni pamoja na huduma za kibingwa za magonjwa ya wanawake, ukunga, huduma za kibingwa za magonjwa ya watoto na watoto wachanga, huduma za kibingwa za upasuaji wa mfumo wa mkojo, huduma za kibingwa za magonjwa ya kinywa na meno na huduma za kibingwa za magonjwa ya ndani" amefafanua Katibu Tawala Makungu.
Bw. Makungu ametumia wasa huo kwa kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma za kibingwa zinazotarajia kutolewa kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 19 hadi 24 Mei 2025 katika zote za Wilaya z mkoa huo.