Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

KALIUA WACHANGAMKIA HUDUMA YA MADAKTARI BINGWA,

Posted on: June 13th, 2024


Na WAF, Kaliuwa, TABORA


Wananchi wilayani Kaliuwa mkoani Tabora, wamejitokeza kwa wingi kwenye Kambi ya Madaktari Bingwa na Bobezi waliokita kambi ya Siku Nne wilayani hapo.


Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Dkt. Irene Apina amesema wananchi waliojitokeza ni mara tatu ya wagonjwa katika siku za kawaida.


Dkt. Irene Apina ameiomba Serikali wanaposoma Bajeti kuu ya Serikali basi suala la Afya lipewe kipaumbele.


“Tumeona watu zaidi ya 300 kwenye hizi siku tatu, hii ni ishara kwamba watu wana matatizo lakini wanashindwa kufikia huduma za kibingwa, amesema Iren na kuongeza


“Unaweza kumuandikia mgonjwa rufani aende Kitete lakini anarudi nyumbani, hivyo ujio wa Madaktari Bingwa ni fursa kwa wananchi wetu” amesema Irene.


Dkt. Irene ameiomba Serikali kutoa kipaumbele cha bajeti kwenye masuala ya afya kwani uhitaji wa watumishi ni asilimia 31 ili kuziba mapengo yaliopo hivyo bajeti ikitoa kipaumbele kwenye afya itakuwa ni faraja kwao.


Daktari Bingwa wa Upasuaji, Ahmed Binde kutoka Bugando aliyepo katika jopo hilo amwsema idadi kubwa ya wananchi wa Kaliuwa wanakabiliwa na upungufu wa damu.


“Tumetumia fursa hii kutoa elimu ya lishe Bora ili kukabilina na hali ya upungufu wa damu inayo wakabili kwani watu wengi wanakula Udongo na ndani udongo kuna minyoo ya aina tofauti hivyo lazima wananchi walijue hili” amesema Dkt. Binde


Kwa upande wa wananchi wa Kaliuwa wameishukuru Serikali kwa hatua yakuwasogezea huduma hiyo.


Akizungumza Hospitalini hapo Bi Frida Titto, amesema wanaiomba serikali kuifanya huduma ya mkoba iwe endelevu huku akiitaka Serikali kuweka kipaumbele kwenye Bajeti.

MWISHO