Dkt. Mollel akoshwa na Kambi ya Madaktari Bingwa na bobezi Arusha
Posted on: June 29th, 2024
Na.WAF, Arusha
Kutokana na watu wengi kujitokeza katika Kambi ya matatibabu katika uwanja wa Sheikhe Amri Abeid Jijini Arusha Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel amesema kuna haja ya madaktari kushuka chini zaidi ili kuwafikia watanzania wengi kama alivyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan.
Madaktari bingwa na wataalamu wa afya zaidi ya 500 kutoka hospitali na Taasisi mbalimbali za afya hapa nchini, wanatoa huduma ya vipimo, matibabu na dawa bure katika uwanja wa Sheikhe Amri Abeid kuanzia Juni 24 mpaka Julai mosi mwaka huu.
Akizungumza wakati alipotembelea Kambi hiyo, Dkt.Mollel ameeleza kuwa Rais Samia alimwita Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu na yeye na kuwapa maelekezo ya kuhakikisha watanzania wengi wanafikiwa na huduma za afya.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo mahususi kwamba madaktari washuke chini kuwafuata wagonjwa jambo ambalo wamekuwa walikifanya katika maeneo mbalimbali.
Amesema wamekuwa wakizunguka katika Wilaya sio kutibu pekee bali na kuwajengea uwezo watu wa Hospitali za Wilaya.
Amesema kwenye eneo la ugonjwa wa kansa wameona miaka miwili iliyopita ukienda Ocean Road asilimia 80 ya wagonjwa ni wale ambao wanangojea kufa.
Dkt.Mollel amesema baada ya maelekezo ya Rais na Teknolojia aliyoishusha chini ya kununua vifaa sasa hivi zaidi ya asilimia 78 ya wagonjwa wanapokuja wanakuja mapema na wanagundulika mapema na wanapona.
Amesema madaktari bingwa wamezunguka katika Mikoa mbalimbali na kwa sasa wapo Jijini Arusha.
"Na kwa kweli tumpongeze Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda, madaktari katika Hospitali zetu za Taifa na tuupongeze Mkoa wa Arusha.
Amesema hiyo ni programu maalum ijulikanayo kwa jina la Kibingwa ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.
"Maana yake ukimwona daktari ujue analipwa.Lakini nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Arusha wametoka wananchi wengi na yeye akajiongezea
Kuhusu Kambi ya matibabu amesema mpaka wametibiwa wananchi 28976 na ambao wanatakiwa kwenda Rufaa Muhimbili ni 700.
"Na tunaye daktari wa matatizo ya moyo na watatakiwa kwenda 200 wanahitaji kusaidiwa," ameeleza Dkt.Mollel
Amesema kwa Mkoa wa Arusha ambao wametoka Wilayani waliotibiwa ni 466 ambapo mpaka Jumatatu wananchi wengi watafika kupatiwa matibabu.
Amesema tathmini ni kwamba watu 28,000 wameshindwa kupata huduma kwa utaratibu wa kawaida.
Amesema wanahitaji kuongeza nguvu katika Mkakati wa Rais Samia Suluhu Hassan na madaktari wanatakiwa kushuka chini zaidi.
Tunahitaji kuongeza nguvu katika Hospitali Wilaya.Inatupa alamu kwamba suala la bima ya afya kwa wote hiyo ni kipaumbele.Bima ni njia ya kudundiliza ili likitokea tatizo uweze kuhudumia njia yetu ya kuchangiana kikubwa wote tuhamaishane suala kubwa ni bima ya afya,"amesema Dkt.Mollel
Pia amesema suala la usalama barabarani ni suala la msingi kwa watu wote huku akidai magonjwa mengi yanatokana na namna watu wanavyoishi na Vyakula wanavyokula.
"Kila mtu aanze kufikiria aina ya style ya maisha na anapoendesha chombo cha moto anaendeshaje,"amesema Dkt. Mollel