WIZARA, WADAU WAKUTANA KUPITIA MKAKATI WA MAWASILIANO WA HUDUMA ZA CHANJO NCHINI
Posted on: September 11th, 2025
Wizara ya Afya pamoja na wadau wa kisekta wako mkoani Morogoro kwenye kikao kazi cha siku tano kwa ajili ya kuboresha na kuuhisha taarifa kwenye mkakati wa mawasiliano utakaotumika katika uhamasishaji wa huduma za chanjo nchini.
Mkakati wa Mawasiliano wa huduma za chanjo nchini unafanyiwa maboresho baada ya kutumika kwa miaka mitano ili kuendana na hali ya sasa ya utoaji huduma za chanjo nchini.
Mkakati huo unaosimamiwa na Idara ya Kinga kupitia Mpango wa Taifa wa huduma za Chanjo unalenga kuwafikia viongozi wa Dini, Wananchi kwa kushirikiana na Maafisa Afya ngazi ya Jamii na vyombo vya habari.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Septemba 10, 2025, Mkuu wa Mafunzo na Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa Chanjo Bi. Lotalis Gadau amewataka wajumbe wa kikao kujielekeza zaidi katika kuboresha mkakati huo ili uendane na mazingira ya kisasa ya utoaji huduma za chanjo.
Wadau wa kikao kazi ikiwemo Ofisi ya Rais TAMISEMI tayari wameboresha taarifa muhimu za utoaji elimu huduma ya chanjo kama hatua muhimu ya kujipanga kutoa elimu kwa umma kuhusu chanjo zilizopo na zitakazoendelea kutolewa.