Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WAZIRI MHAGAMA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA FALME YA ESWATINI

Posted on: April 16th, 2025

Waziri wa Afya na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jenista Mhagama leo Aprili 15, 2025 amewasilisha ujumbe maalum kwa Falme ya Eswatini ambao umepokelewa na Waziri Mkuu wa Falme hiyo Mhe. Russell Mmiso Dlamini Jijini Mbabane, Eswatini.


Waziri Mhagama ameushukuru Falme ya Eswatini kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendeleza ushirikiano mzuri wa Kidiplomasia uliopo baina ya Mataifa hayo mawili.


Waziri Mhagama ameambatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji anayewakilisha Tanzania pia katika Falme ya Eswatini, Mhe. Ali Ubwa Mussa pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace, Magembe.