Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WATUMISHI WATAKIWA KUTUNZA VIFAA VYA HUDUMA

Posted on: September 19th, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi kutunza vifaa vya kutolea huduma za afya kwa wananchi kwani vimeigharimu Serikali fedha nyingi.


Rais Samia amesema hayo leo tarehe 19 Septemba 2023 wakati akiweka jiwe la msingi katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.


Hospitali hiyo imegharimu shilingi  Bilioni  4.8 katika ujenzi wake pamoja na ununuzi wa Vifaa na tayari mpaka sasa  imeshatoa huduma ya CT Scan kwa wananchi 108.


Aidha, uwekaji  wa  jiwe la msingi  katika  Hospitali hiyo umeenda sambamba na utoaji wa huduma  za wagonjwa wa nje (OPD), Huduma za wagonjwa wa dharura (EMD), huduma za Radiolojia pamoja na huduma za CT Scan hivyo kuwaondolea kero wananchi wa mkoa huo kusafiri mwendo mrefu kufuata  huduma hizo.