Ministry of Health

WATAALAMU WA AFYA WAKUTANA KUANDAA MWONGOZO WA UFUATILIAJI VISABABISHI VYA UCHAFUZI WA MAZINGIRA VYENYE MADHARA KWA JAMII.

Posted on: April 20th, 2026

Na Mvuda Jaffer, WAF – Morogoro

Wizara za Afya Bara na Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia mradi wa kupambana na majanga (Pandemic Fund) imekutanisha timu ya wataalamu wabobezi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ili kuandaa rasimu ya mwongozo wa ufuatiliaji wa viashiria vya uchafuzi wa mazingira vinavyoathiri afya ya jamii.

Akizungumza katika kikao kazi hicho Aprili 15, 2026 Mkoani Morogoro Mkuu wa Huduma za Afya Mipakani, Dkt. Remidius Kakulu amesisitiza umuhimu wa kuandaa mwongozo huo ambao utasaidia mamlaka za afya katika ngazi ya Halmashauri na Mipakani kufuatilia na kudhibiti mapema hatari za uchafuzi wa mazingira ili kulinda jamii na magonjwa ya milipuko na yale yasiyokuwa ya kuambukiza.

“Mwongozo huu pia ni takwa la sheria ya afya ya jamii ya mwaka 2009 nasheria za kimataifa za mwaka 2009, hivyo ufuatiliaji wa viashiria vya mazingira ni nguzo muhimu katika kuzuia kuenea kwa magonjwa na kulinda afya ya wananchi,” amesema Dkt. kakulu.

Naye Mkuu wa huduma za Afya Mipakani kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Rukaiya Mohamed Said ameeleza kuwamwongozo huu ni muhimu pia kwa upande wa Zanzibar kwani visababishi vya uchafuzi wa mazingira ni vilevile hatakwa upande wa Zanzibar.

Amebainisha kuwa Zanzibar imewakilishwa kikamilifu  na wataalamu kutoka sektambalimbali ikiwema mamlaka ya udhibiti wa MazingiraZanzibar (ZEMA), Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), wataalamu kutoka wizara ya afya sehemu ya afya mazingirana huduma za Afya mipakani.

Pia, Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani Dkt. George Kauki ameeleza kuwa WHO itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarishamifumo ya Ufuatiliaji wa magonjwa ili kubaini mapemaviashiria vinaweweza kusababisha uchafuzi wa mazingira nakuvidhibiti visiweze kuleta madhara kwa Afya ya Jamii.

Naye Bi. Suzana Nchalla, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema kuwamwongozo huu ukikamilika utasaidia Maafisa Afya katikangazi za halmashauri kuimarisha ufuatiliaji wa uchafuzi wa mazingira na utambuzi wa mapem