Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WATAALAM WA MAABARA KUJENGEWA UWEZO KUDHIBITI KIPINDUPINDU NCHINI.

Posted on: October 16th, 2025

Na, WAF - Dar es salaam

Serikali kupitia Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii imejipanga kuimarisha ufuatiliaji na kuwajengea uwezo wataalam wa afya nchini ili kuboresha utambuzi wa haraka wa ugonjwa wa Kipindupindu, hatua itakayosaidia kuudhibiti kabla haujasambaa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Oktoba 16, 2025, wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa miaka miwili ya Mradi wa Kujengea Uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, unaofadhiliwa na Shirika la Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH), Kaimu Mkurugenzi wa Maabara hiyo, Bw. Ambele Mwafulango, amesema mpango wa mwaka wa tatu wa mradi huo umejikita katika kujenga uwezo wa wataalam katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema lengo ni kuhakikisha wataalam hao wanaweza kutambua mapema viashiria vya ugonjwa wa kipindupindu kabla ya kuzuka kwa mlipuko, hasa kutokana na ugonjwa huo kuripotiwa mara kwa mara katika maeneo tofauti nchini.

“Mradi wa kujengea uwezo wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii unaofadhiliwa na KOFIH ni wa miaka mitano. Leo tumefanya tathmini ya miaka miwili na kuweka mikakati ya mwaka wa tatu, ambapo tutajikita zaidi kwenye kipindupindu, huku tukiendelea na tafiti za magonjwa ya mfumo wa upumuaji,” amesema Bw. Mwafulango.

Ameongeza kuwa awamu inayofuata itahusisha mafunzo kwa wataalam wa maabara katika mikoa mbalimbali nje ya Dar es Salaam, ili kuwawezesha kutambua mapema visa vya kipindupindu, kufuatilia wagonjwa kwa karibu, na kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la KOFIH nchini Tanzania, Dkt. Hansol Park, amesema shirika hilo linaendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya kipindupindu kwa kuimarisha uwezo wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii.

“Tunaunga mkono juhudi za Serikali kwa sababu idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imekuwa ikiripotiwa katika maeneo mbalimbali. Lengo letu ni kusaidia utambuzi wa mapema na udhibiti wa ugonjwa huo,” amesema Dkt. Park.

Naye Mshauri Muelekezi wa Mradi huo, Prof. Jeremia Semi, amesema dunia kwa sasa imejikita katika kupambana na magonjwa ya milipuko ambayo ni tishio la kimata