Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WANANCHI NKASI WAITIKIA UJIO WA MADAKTARI BINGWA

Posted on: October 3rd, 2025

NA WAF - RUKWA

Wananchi wa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wamejitokeza kwa wingi kupata huduma za kibingwa kufuatia ujio wa timu ya madaktari bingwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 01, 2025 na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi, Dkt. Benjamin Ndeule wakati wa kambi ya madaktari Bingwa wa Rais Samia, mkoani Rukwa.

“Muitikio huo mkubwa umetokana na hamasa na matangazo yaliyotolewa mapema na viongozi wa afya pamoja na vyombo vya habari, hali iliyosaidia kuwafahamisha wananchi kuhusu fursa hiyo ya kipekee,” amesema Dkt. Ndeule.

Madaktari bingwa hao wanatoa huduma kwa wananchi wenye magonjwa mbalimbali yakiwemo ya moyo, macho, upasuaji, wanawake na watoto.

Mganga Mkuu wa Wilaya amepongeza muitikio huo mkubwa, akisisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni kielelezo cha uelewa na thamani wanayoipa afya yao na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha huduma bora zinawafikia watu wote mahali walipo.

Wananchi waliopata huduma wameeleza kufurahishwa na huduma hizo, huku wakitoa shukrani kwa Serikali na wadau wa afya kwa kuwaletea madaktari bingwa katika wilaya yao, jambo linaloonyesha nia ya dhati ya serikali ya kuboresha sekta ya afya nchini. WANANCHI NKASI WAITIKIA UJIO WA MADAKTARI BINGWA

NA WAF - RUKWA

Wananchi wa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wamejitokeza kwa wingi kupata huduma za kibingwa kufuatia ujio wa timu ya madaktari bingwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 01, 2025 na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi, Dkt. Benjamin Ndeule wakati wa kambi ya madaktari Bingwa wa Rais Samia, mkoani Rukwa.

“Muitikio huo mkubwa umetokana na hamasa na matangazo yaliyotolewa mapema na viongozi wa afya pamoja na vyombo vya habari, hali iliyosaidia kuwafahamisha wananchi kuhusu fursa hiyo ya kipekee,” amesema Dkt. Ndeule.

Madaktari bingwa hao wanatoa huduma kwa wananchi wenye magonjwa mbalimbali yakiwemo ya moyo, macho, upasuaji, wanawake na watoto.

Mganga Mkuu wa Wilaya amepongeza muitikio huo mkubwa, akisisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni kielelezo cha uelewa na thamani wanayoipa afya yao na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha huduma bora zinawafikia watu wote mahali walipo.

Wananchi waliopata huduma wameeleza kufurahishwa na huduma hizo, huku wakitoa shukrani kwa Serikali na wadau wa afya kwa kuwaletea madaktari bingwa katika wilaya yao, jambo linaloonyesha nia ya dhati ya serikali ya kuboresha sekta ya afya nchini.