SERIKALI YAONGEZA KASI MPAMGO WA MMS KULINDA AFYA YA MAMA NA MTOTO
Posted on: February 14th, 2026Na WAF - Dar es Salaam
Wizara ya Afya inaendelea kuimarisha huduma za lishe kwa mama wajawazito kwa kuongeza matumizi ya virutubishi mchanganyiko (Multiple Micronutrient Supplements – MMS) ili kuboresha afya ya mama wajawazito na watoto wachanga.
Huduma hizo zinaendelea kuimarishwa kwa kutoa mafunzo yanafanyika jijini Dar es Salaam wiki hii ambayo yamewakutanisha wadau kutoka Serikalini na taasisi zisizo za Kiserikali zinazosaidia uboreshaji wa lishe na afya ya umma ikiwemo Africa Academy for Public Health(AAPH), Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC), Ifakara Health Institute (IHI), Muhimbili University of Health na Allied Sciences (MUHAS).
Baadhi ya taasisi shiriki ni pamoja na Africa Academy for Public Health, Tanzania Food and Nutrition Centre, Ifakara Health Institute na Muhimbili University of Health and Allied Sciences, zikishirikiana na Wizara ili kuhakikisha mpango huo wa MMS unatekelezwa kwa ufanisi na uendelevu.
Ili kuhakikisha utekelezaji wenye ufanisi, Wizara imeandaa mafunzo hayo maalum ya kukadiria gharama za utekelezaji wa mpango huo kwa kuangalia uhalisia wa Tanzania na kuzingatia mifumo ya afya iliyopo, rasilimali zinazopatikana na uwezo wa utekelezaji wa nchi.
Mpango wa MMS unalenga kupunguza changamoto za watoto kuzaliwa na uzito mdogo, kuzaliwa kabla ya muda, pamoja na vifo vya watoto wachanga, hivyo kuongeza nafasi ya mtoto kuishi na kukua kwa afya njema.