SERIKALI ,WADAU KUENDELEA KUWEKEZA KUIMARISHA UCHUNGUZI WA MAABARA NA MAPAMBANO DHIDI YA UVIDA.
Posted on: May 19th, 2026Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia Mradi wa Pandemic Fund imeendelea kuwekeza katika kuimarisha huduma za uchunguzi wa maabara na matumizi sahihi ya dawa, hususani antibiotiki, ili kudhibiti ongezeko la vimelea vinavyoshindwa kutibika kwa dawa zilizopo sasa.
Akizungumza Mei 19, 2026 mkoani Morogoro Mratibu wa Taifa wa UVIDA, Bi. Emiliana Francis, wakati wa mwendelezo wa kikao kazi cha uandaaji wa mpango kazi wa ufuatiliaji wa usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, kinachowakutanisha wataalamu kutoka sekta ya afya ya binadamu na mifugo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
“Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani kupitia Mradi wa Pandemic Fund imedhamiria kuimarisha huduma za uchunguzi wa vimelea vya magonjwa ili kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu sahihi na kupunguza janga la usugu wa vimelea dhidi ya dawa,” amesema Bi. Emiliana.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha ushirikiano wa sekta mbalimbali kupitia mkakati wa Afya Moja (One Health) unaojumuisha sekta ya afya ya binadamu, mifugo na mazingira katika kudhibiti UVIDA hapa nchini.
Amesema kuwa, baadhi ya hatua zinazoendelea kutekelezwa ni pamoja na kuimarisha huduma za uchunguzi katika maabara za afya ya binadamu na mifugo, usimamizi wa matumizi sahihi ya dawa, kudhibiti maambukizi ya vimelea vya magonjwa pamoja na kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu athari za matumizi holela ya dawa.
Kwa upande wake, mwakilishi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Gibonce Kayuni, amesema ushirikiano kati ya sekta ya afya ya binadamu na mifugo ni muhimu katika kudhibiti usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa kutokana na changamoto hiyo kuathiri afya ya watu, wanyama na mazingira kwa pamoja.
Naye Mkuu wa Huduma za Uchunguzi kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Bw. Abdallah Saidi Mohamed, amesema kuimarishwa kwa mifumo ya ufuatiliaji wa UVIDA kutasaidia kuongeza ubora wa huduma za afya na kuhakikisha wananchi wanapata