Customer Feedback Centre

Ministry of Health

RUFAA ZA NJE YA NCHI ZIMEPUNGUA KWA ASILIMIA 97

Posted on: August 11th, 2024



NA WAF, Kilimanjaro

Serikali kupitia wizara ya afya imepunguza rufaa za nje ya nchi kwa asilimia 97 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa Leo Agosti 11, 2024 Mkoani Kilimanjaro na Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na viogozi wa kata 170 katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali imewekeza teknolojia ya kisasa katika Hospitali zote nchini ikiwa ni kutekeleza uboreshaji wa huduma za afya kwa jamii ili kila mwananchi apate huduma bora za afya.

“Tumepunguza rufaa za nje kwa asilimia 97, wanaokwenda nje kwa ajili ya matibabu ni asilimia 3 huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais Wetu ameleta hospitali nzuri na vifaa tiba vya kutosha ili kuleta huduma bora kwa wananchi”. Amesema Dkt Mollel.

Hata hivyo Dkt. Mollel ametoa rai kwa viongozi wa kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa Bima ya afya ili kupunguza makali ya matibabu kwani gharama za matibabu ni kubwa.

“Tuna teknolojia kubwa na nzuri lakini ni muhimu kuwa na Bima ya afya kwa ajili ya kutumia kwenye matibabu, uwekezaji huu ni mkubwa na una gharama kubwa hivyo ukiwa na Bima ya afya itapunguza makali.