Customer Feedback Centre

Ministry of Health

NDANI YA MIAKA MIWILI TUMEJENGA VITUO VIPYA 1498 VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Posted on: October 28th, 2023


Ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan jumla ya vituo vipya 1,498 vya kutolea huduma za afya vimejengwa hapa nchini.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo kwenye Hafla ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuzindua ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria ya mwaka 2022.


“Mwaka 2021 tulikuwa na vituo 10153 leo tuna vituo 11651, ongezeko la vituo 1498 na vingi vimeanza kufanya kazi” amesema Waziri Ummy Mwalimu.


Waziri Ummy amesema kuwa Rais Samia amewezesha ununuzi na usimikaji wa vifaatiba vya kisasa ikiwemo mashine za uchunugzi wa Radiolojia za CT Scan nchi nzima.


“Leo hii hakuna haja tena ya mtu kutoka Kigoma au Katavi kusafiri hadi kuja Dar Es Salaam kwa ajili ya huduma za CT Scan, haya yote umewezesha wewe Rais Samia” amesema Waziri Ummy.