Ministry of Health

NAIBU WAZIRI DKT. SAMIZI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA KIKAO CHA 76 CHA WHO

Posted on: September 25th, 2026

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Florence Samizi anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha 76 cha Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO AFRO Regional Committee), kinachofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 25–28 Agosti 2026.

Kikao hicho kimefunguliwa Rasmi leo Agosti 25, 2026 ambacho kinawakutanisha Mawaziri na viongozi wa afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe na viongozi kutoka Wizara ya Afya Tanzania.

Lengo la kikao hicho ni kujadili masuala muhimu ya afya, ikiwemo kuimarisha mifumo ya afya, usalama wa afya, upatikanaji wa huduma bora na usawa katika huduma za afya barani Afrika.

Ushiriki wa Tanzania unalenga kuendelea kushirikisha uzoefu, kuwasilisha vipaumbele vya nchi na kuchangia katika mijadala na maamuzi yanayolenga kuimarisha afya na ustawi wa wananchi barani Afrika.