Ministry of Health

MUHIMBILI YAZINDUA GARI LA KISASA LA UPASUAJI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA KIBINGWA NCHINI

Posted on: May 20th, 2026

Hospitali ya Taifa Muhimbili imezindua gari maalum la upasuaji la Kwanza na la kipekee kuwahi kuwepo hapa Nchini kwa lengo la kuwezesha utoaji wa huduma za kibingwa za upasuaji katika maeneo mbalimbali ya Tanzania kupitia huduma mkoba.

Akishiriki katika uzinduzi wa gari hilo leo Mei 20, 2026, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, kwa niaba ya Waziri wa Afya mhe. Mohamed Mchengerwa amesema, hatua hiyo ni mafanikio makubwa katika kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi, hususan waliopo maeneo ya mbali ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kufuata huduma za Afya mbali na Hospitalini.

Dkt. Samizi ameipongeza Sokus Kova Foundation kwa kuwezesha upatikanaji wa gari hilo kutoka nchini China, akisema msaada huo utaongeza uwezo wa Serikali kufikisha huduma za afya kwa wananchi wengi zaidi.

“Tunawashukuru sana wenzetu wa Kova Foundation kwa kuhakikisha gari hili maalum linafika mikononi mwa Hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili. Pia tunaishukuru Serikali ya China kwa msaada huu mkubwa kwa sababu sasa tunatoa huduma za upasuaji mahali popote na siyo kulazimika wananchi kufika hospitalini,” amesema Dkt. Samizi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili, Dkt. Delilah Kimambo, amesema gari hilo litasaidia kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali ambao wamekuwa wakikosa huduma za kibingwa kutokana na changamoto za umbali, gharama za usafiri na uhaba wa huduma maalum za upasuaji.

Amesema gari hilo limefungwa teknolojia ya kisasa pamoja na vifaa maalum vya upasuaji vinavyowezesha kutoa huduma mbalimbali zikiwemo operesheni za dharura, uchunguzi wa awali pamoja na huduma za kibingwa za afya.

Aidha, gari hilo lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja ni la kwanza nchini kwa aina yake, na linatarajiwa kusaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa wananchi wa maeneo yasiyokuwa na miundombinu ya kutosha ya afya.

Uzinduzi wa gari hilo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kuimarisha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kupunguza gharama pamoja na