Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MSONGO WA MAWAZO WATAJWA KUWA SABABU YA KUATHIRI AFYA YA WAJAWAZITO NA LISHE KWA WATOTO

Posted on: August 2nd, 2023

Na. Catherine Sungura, Dar es Salaam

Wajawazito nchini wametakiwa kukaa katika mazingira yasiyowaletea msongo wa mawazo katika kipindi chote cha ujauzito na unyonyeshaji ili kufanya maziwa yatoke vizuri na mtoto kupata lishe bora na kukua vizuri

Wito huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel wakati wa uzinduzi wa wiki ya unyonyeshaji inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 1 hadi 8 kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mollel amesema kuwa, mama mjamzito anahitaji matunzo kwaajili ya lishe ya mtoto katika siku 1000 Yaani tangu kutungwa kwa mimba hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili kwani ndio msingi bora wa ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili.

“Katika siku hizi 1000 madhara ya lishe duni hasa udumavu yanaathiri sana maendeleo ya rasilimali watu ya nchi, hivyo ni muhimu mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo na kuendelea kunyonyeshwa huku akipatiwa chakula cha nyongeza hadi anapotimiza miaka miwili au zaidi.” Amesema Dkt. Mollel

Aidha, Dkt. Mollel amesema, watoto wadogo na watu wazima wanapaswa kula lishe bora ili kuwaepusha na magonjwa yanayotokana na kutokula lishe isiyokamilika.

“Kuna magonjwa mengi yanayotokana na kutokula lishe kamili ni vyema watoto na watu wazima kuzingatia hilo, pia lishe inayozidi inasababisha uzito uliozidi na hivyo kusababisha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Figo na moyo.”Alisisitiza Dkt. Mollel

Kuhusu takwimu za lishe Naibu Waziri alisema, asilimia ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee imeongezeka kutoka 58% mwaka 2018 hadi kufikia 64% mwaka 2022.

Vile vile takwimu ya watoto wanaonyonyeshwa ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa imeongezeka kutoka 53.5% mwaka 2018 hadi kufikia 70% mwaka 2022.

Hata hivyo Dkt. Mollel amewahimiza waajiri katika Sekta rasmi na zisizo rasmi na jamii kwa ujumla kuwasaidia wanawake waweze kunyonyesha watoto wao huku wakiendelea kufanya kazi na kuwakumbusha viongozi, wasimamizi, Wataalamu na watendaji kuendelea kuelimisha umma kuhusu sheria ya kulinda haki za uzazi kwa wanawake pamoja na kuwahimiza waajiri kutenga sehemu maalum