MJADALA KITAIFA KUWEKA VIPAUMBELE UFADHILI WA MFUKO WA DUNIA KUKABILI UKIMWI, KIFUA KIKUU NA MALARIA MZUNGUKO WA NANE (GC8) WAZINDULIWA
Posted on: April 8th, 2026Na WAF, Dar es Salaam
Serikali ya Tanzania imezindua rasmi Mjadala wa Kitaifa (Country Dialogue) wa siku mbili kwa ajili ya kuandaa andiko la kuomba fedha kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria Mzuko wa nane (Grant Cycle 8 - GC8).
Hatua hii inalenga kuhakikisha wadau wote wanafanya mjadala na kuja na vipaumbele vitakavyozingatiwa katika andiko la kuomba fedha kupitia ufadhili huo kwa ajili ya mapambano ya magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria kwa kipindi cha utekelezaji cha kuanzia Januari Mosi, 2027 hadi Desemba 31, 2029.
Akifungua kikao cha siku mbili Aprili 8, 2026 Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amesema tukio hilo ni fursa muhimu ya kuonyesha vipaumbele vya kitaifa vinavyotokana na mjadala baina ya Serikali, Wadau wa Maendeleo,Watekelezaji, jamii na wadau wote.
"Ushirikiano huu unaonyesha dhamira thabiti ya kusikiliza sauti zote na kuhakikisha maamuzi yanayofanywa yanaleta faida kwa nchi," amesema Dkt. Shekalaghe.
Amefafanua kuwa, katika wiki mbili zilizopita, zaidi ya wawakilishi 130 wa mashirika yasiyo ya kiserikali walikutana kujadili vipaumbele vya jamii, makundi muhimu, na mifumo ya jamii. Pia, zaidi ya wawakilishi 120 wa serikali kutoka mikoa mbalimbali walishiriki kikao cha kuainisha vipaumbele vya kitaifa kulingana na sera, ushahidi wa kisayansi na hali halisi za programu.
Dkt. Shekalaghe amesema huu si mkutano wa kawaida, bali ni juhudi za kimkakati zisizo na upendeleo ili kuhakikisha hakuna sauti inayoachwa nyuma.
Tanzania imepatiwa takriban USD 538.6 milioni kwa kipindi cha 2027–2029 kufanikisha programu za HIV, TB na malaria. Hii ni fursa ya kipekee ya kuharakisha maendeleo na kuziba mapengo muhimu kwenye huduma za afya, lakini pia ni wajibu wa kuhakikisha kila dola inatumika kwa mikakati yenye tija, uwazi, na matokeo kwa wananchi.
Mjadala huu kuelekea kuandaa andiko la GC8 unalenga kufikia mabadiliko makubwa katik