Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MIFUMO ISOMANE KULETA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA ZA MIFUKO YA BIMA YA AFYA NCHINI

Posted on: October 11th, 2023


Na. WAF, Dodoma

NAIBU Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel amesisitiza mifumo ya matibabu kuanzia ngazi ya vituo vya afya hadi ngazi ya Hospitali za Taifa isomane ili kupumguza matumizi mabaya ya fedha za Mifuko ya Bima ya Afya nchi.


Dkt. Mollel ametoa wito huo leo jijini Dodoma wakati akipokea mradi wa uimarishaji wa huduma za afya (HPSS) iliokuwa ukitekelezwa nchini kwa ufadhili wa serikali ya Uswiswi.


Ameeleza kuwa kutokana na mifumo kutokusomana husababisha mgonjwa kurudia vipimo bila sababu ya msingi pale anapopewa rufaa kwenda hospitali nyingine.


“Tunahitaji kufika mahali mifumo ya afya isomane katika ngazi zote itasaidia kupuguza matumizi mabaya ya fedha za mfuko wa bima ya afya kwasaabu hakutakuwa na haja ya kurudia vipimo pasipo kuwa na sababu ya msingi”, amesisitiza Dkt. Mollel.


Hata hivyo ameongeza kuwa kwasasa nchi inaelekea kwenye mfumo wa bima ya afya kwa wote hivyo watakuwa makini kutokutumia fedha kwenye mambo ambayo sio ya msingi ndio maana wananasisitiza mifumo isomae ili bima ya afya kwa wote kufanya kazi kwa ufanisi.




Aidha Dk.Mollel amesisitiza kuwa katika utekelezaji wa mradi wa HPSS awamu ya pili ni vyema makubaliano yajikite kwenye bima ya afya kwa wote kwani dhamira ya serikali na kipaumbele cha Wizara ya Afya ni kuhakikisha kila mwaachi anapata Huduma bora za afya bila kikwazo.


Naye Meneja Mradi wa HPSS – Tuimarishe Afya Ally Kebby amesema suala la Bima ya afya kwa wote wanasubiri utaratibu watakao patiwa na serikali na kama wadau wameahidi kuendana na mpango huo ili kuhakikisha serikali inatimiza malengo yake kwatika kuwahudumia wananchi.


Kebby amesema maeneo manne ambayo mradi wa HPSS umefanikiwa kufkiia malengo yake waliyopewa ya kufanyia maboresho mfuko wa afya ya jamii kuwa bima ya afya na hilo limefanyika kwa kushirikiana na wadau wengine na sasa mfumo huo unatekelezwa na serikali yenyewe.


“Tulipewa jukumu la kuhakikisha tunakuja na ugunduzi mzuri wa afua zitakazosaidia kuboresha upatikanaji wa dawa na kuboreshausimamizi wa matumizi ya dawa,tumefanya kazi hiyo pamoja na wizara mbili ya Afya na TAMISEMI, na sasa tumeweza kutengeneza mifumo ya ugavi wa dawa lakini utaratibu wa menejimenti na usimamizi wa dawa kwenye vituo”, amebainisha Kebby


Ameongeza kuwa wamefanikiwa kuimarisha mifumo rasmi ya utoaji wa huduma ambapo serikali imekuwa na utaratibu wa kushirikisha wadau katika kuainisha afua na shughuli zinazoendana na vipaumbele kwa sasa wanasubiri muongozo kutoka serikalini kuhusu utekelezaji wa Bima ya afya kwa wote ili waweze kuangalia ni kwa namna gani watakavyoshiriki kufanikisha utaratibu huo