Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA CHANGAMOTO AFRIKA

Posted on: November 13th, 2023


Imeelezwa kuwa magonjwa yasioambukiza imekuwa changamoto Barani Afrika ikiwemo shinikizo la damu (presha) na Kisukari.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Magonjwa yasioambukiza Wizara ya Afya Dkt. Omary Ubuguyu katika uzinduzi wa madhimisho ya wiki ya magonjwa yasioambukiza iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Ofisi ya (TAMISEMI) uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam pamoja na wadau wa huduma za magonjwa yasioambukiza.


“Magonjwa yasioambukiza yamekuwa ni changamoto kubwa hasa katika Bara letu la Afrika ikiwemo Kisukari na Shinikizo la damu, “amesema Dkt Omary.


Dkt. Omary amesema utafiti unaeleza katika watu 100 watu watano wana ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la damu hivyo amewataka wananchi kushiriki mazoezi na kuweka mpangilio wa vyakula kiafya.


Aidha Dkt.Omary amesema utafiti unaeleza kuwa umri wa kuishi kwa wanawake ni miaka 69 na wanaume umepungua kwa sasa wanaishi miaka 62 kwa ajili ya changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi,mazingira na mabadiliko katika maendeleo.


Pia amesema magonjwa yasioambukiza changamoto hasa katika umri wa wazee ndio maana katika maadhimisho hayo ya wiki ya magonjwa yasioambukiza wamewashirikisha wazee na kuwakumbusha kufanya mazoezi ya kukunja misuri kwani mazoezi ya mara kwa mara yanasaidia kutoa sumu mwilini na kuimarisha mifupa na nyonga


Amewataka wafanye ibada kila wakati pia ni sehemu ya mazoezi na ujenga afya huku akitoa agizo kwa vituo vya afya vyote kutoa huduma za upimaji afya kwa wananchi ambapo madhimisho hayo yanatarajia kufungwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Mganga Mkuu Mkoa Dar es Salaam Rashid Mfaume amesema siku ya Magonjwa yasioambukiza Kitaifa mwaka huu yatafanyika Mkoa Dar es Salaam Novemba 14 mpaka 18 ambapo magonjwa mbalimbali yatapimwa viwanja vya Mnazi Mmoja na madaktari bingwa watakuwepo.


Dkt Rashid Mfaume amesema Wazee ni tunu kubwa sana katika nchi yetu hivyo ndio maana Serikali inawatumia katika shughuli mbalimbali


Cc. Hari Shaaban - Times Majira Online,Ilala