Customer Feedback Centre

Ministry of Health

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AFUNGA OFISI DAR ILI VIONGOZI WATII AGIZO LA KUHAMIA DODOMA

Posted on: December 23rd, 2022


Na. WAF- Dar es Salaam, 23/12/2022

Menejimenti ya Wizara ya Afya chini ya Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi imechukua hatua za kuifunga Ofisi ya Uratibu wa Miradi wa Ukimwi, TB na Malaria (COAg) iliyopo chini ya Wizara ya Afya ambayo inasimamiwa na Dr Peter Mgosha kwa kukaidi agizo la Rais na Waziri Mkuu kuhamia makao makuu Dodoma.

Prof. Makubi amebainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Dkt. Mgosha amekaidi zaidi ya mara tatu agizo la kuhamia Dodoma pamoja na kukumbushwa na Menejimenti ya Wizara.

Katibu Mkuu ameagiza watumishi wote wa ofisi hiyo wafike Dodoma Jumatatu bila kukosa.

Menejimenti imechukua hatua ya kufunga ofisi hiyo na hatua zingine za kinidhamu ziendelee chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu.