Customer Feedback Centre

Ministry of Health

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KIMATAIFA

Posted on: August 4th, 2023

Wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wanashiriki maonesho ya 95 ya kilimo cha biashara Lusaka Zambia ili kufikia azma ya kutangaza tiba utalii kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

Hayo yamebainishwa na kiongozi wa msafara akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Lazaro Mboma wakati akizungumza na waandishi wa habari Lusaka Zambia.

Amesema kuwa Hospitali imepata fursa ya kushiriki maonyesho hayo ili kutangaza huduma za kibingwa zaidi ili kuweza kuleta wagonjwa wao kupata matibabu kwa ufanisi zaidi badala ya kwenda mataifa ya mbali kwani Tanzania inatumia teknolojia ya hali ya juu katika matibabu kwa sasa.

“Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya inasifika kwa vifaa vya kisasa na wataalamu wa matibabu waliobobea, inatarajia kuvutia wageni wengi zaidi katika lango kuu la kiuchumi katika nchi zilizoko Kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) kwa kuangazia ubora wa huduma za afya zinazopatikana katika hospitali yetu”, ameeleza Dkt. Mboma

Aidha , Dkt Mboma amesema kuwa mpango huo ni sehemu ya kampeni pana yakukutana na wadau kutoka nchi mbalimbali zilizohudhuria ili kutangaza teknolojia ya kisasa katika sekta ya afya mkoani Mbeya na maeneo jirani.

“Tunatarajiwa kuwa na matokeo chanya katika uchumi wa ndani ambapo nchi ya Tanzania kwa uzuri wake wa asili na urithi tajiri wa kitamaduni, Mbeya inakuwa mahali pa lazima kutembelewa na wasafiri kutoka ulimwenguni kote”, ameongeza Dkt. Mboma.

Vile vile, Dkt. Mboma amesisitiza kuwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya itaendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa Tanzania na nchi Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pia kuwa tayari kushirikiana na nchi nyingine katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa mataifa hayo.

Hata hivyo, ameweka wazi kuwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya inatoa huduma za kibingwa na vipimo mbalimbali zikiwemo huduma za upasuaji wa kibingwa kama vile upasuaji wa moyo, ubongo ,uti wa mgongo, figo, ini, upasuaji mdogo, matibabu ya saratani, huduma za magonjwa ya afya ya akili, matibabu ya kisaikolojia