Customer Feedback Centre

Ministry of Health

HALMASHAURI ZIAJIRI WATUMISHI WA MIKATABA KWA MAPATO YA NDANI

Posted on: February 28th, 2024



Na. WAF - Lindi

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri ikiwemo ya Wilaya ya Kilwa kuajiri watumishi wa mikataba kwa kutumia mapato ya ndani ili kupunguza changamoto za uhaba wa wataalamu wa Afya katika Wilaya hizo.

Waziri @ummymwalimu amesema hayo Februari 28, 2024 baada ya kupokea taarifa ya hali ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya hiyo iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Lusajo Mwakajoka ambayo inaonyesha hali ya upatikanaji wa huduma za Afya katika Mkoa wa Lindi, upatikanaji wa Vifaa na Vifaa Tiba pamoja na changamoto.

“Tutatumia njia kuu Tatu ili kupunguza changamoto za watumishi ikiwa ni pamoja na njia ya vibali vya ajira kutoka Ofisi ya Rais Utumishi, kuajiri watumishi kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na kuwataka wadau wetu wa maendeleo katika Sekta ya Afya nao kuhakikisha wanaajiri watumishi wa Afya kwa mikataba ili kutatua changamoto hii kubwa ya uhaba wa Watumishi.” Amesema Waziri Ummy

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amemshukuru Waziri wa Afya Mhe. Ummy kwa kufanya ziara katika Mkoa huo na kumuomba aupe kipaumbele kwa kuwa una wananchi wengi wa kipato cha chini ambao hushidwa kufata huduma mbali na makazi yao.

“Vifaa tiba ikiwemo Dawa zinaposambazwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) tunaomba wawe wanawahi kwa wakati kwa kuwa wananchi wengi wa Mkoa wa Lindi wanakipato cha chini, dawa zinapochelewa tunamkwamisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa ameshatoa fedha za dawa, kikubwa ni sisi watendaji.” Amesema Mhe. Telack

Waziri Ummy anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Lindi na anatarajia kutembelea na kukagua hali ya utoaji wa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi (Sokoine), Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy ameambatana na timu kutoka Wizara ya Afya akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa Dkt. Caroline Damian anae muwakikisha Mkurugenzi wa huduma za Tiba, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu upande wa Hospitali za Rufaa za Mikoa Bw. Danny Temba