Customer Feedback Centre

Ministry of Health

DKT.MOLLEL AFANYA KIKAO NA UONGOZI WA AGA KHAN KWA LENGO LA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI.

Posted on: October 9th, 2023



Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amekutana na uongozi wa Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar Es Salaam na kufanya kikao chenye lengo la kutatua changamoto zinazo wakabili katika kufikia adhima ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Utalii tiba.


Aidha Dkt. Mollel amewapongeza Hospital ya Aga Khan kwa kuendelea kuwahudumia watanzania na wananchi kutoka mataifa mbalimbali wanaofata Huduma za afya hapa nchini .


Amewatia moyo wakuendelea kufanya kazi kwa kutoa Huduma bora zinazo sitahili ili kufikia lengo la Utalii tiba na kuendelea kuvutia mataifa mengine katika kuja kufata Huduma za afya nchini


Pia ameeleza kuwa anawashukuru sana kwa kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania kwa kupokea wataalamu mbali mbali kutoka mataifa mengine kuja kuja kupata ujuzi wa matuibabu ya kibingwa na bobezi Tanzania


“Sisi kama serikali tutaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha Huduma bora za afya nchini zinapatikana na zinakuwa chachu ya kuvutia mataifa mengine kuja kuoata Huduma za kibingwa na bobezi hapa nchini”, ameeleza Dkt. Mollel