Customer Feedback Centre

Ministry of Health

CHW WAMEKUWA MKOMBOZI WA AFYA KWENYE JAMII-BEREGE

Posted on: September 12th, 2025

Na WAF, Rufiji


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya  ya Rufiji Bw.Simon Berege amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii(CHW's) wamekuwa mkombozi wa huduma za afya katika jamii.




Bw. Berege amesema hayo leo Septemba 12, 2025 wilayani Rufiji mara baada ya Wizara ya Afya Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Bara, OR- TAMISEMI na Mdau AMREF chini ya mradi wa Saving lives and Livelihoods (Mastercard Foundation) kufanya ziara ya kubadilishana uzoefu kwa wahudumu wa afya Ngazi ya Jamii kutoka Zanzibar.


"CHW wamekuwa mkombozi mkubwa kwenye eneo la afya katika nyanja mbalimbali ikiwemo huduma za rufaa, hivyo niwapongeze wenzetu kutoka Zanzibar kwa kuja kuona namna uratibu wa CHW unavyofanyika, "amesema Bw. Berege.


Lengo la ziara hiyo ni kubadilishana uzoefu na kujifunza namna gani  Serikali ilivyofanikiwa kuwatumia CHW Bara kwenye utoaji wa huduma za chanjo na huduma nyingine za afya.


Ziara inafanyika kwa siku tatu katika  mikoa ya Pwani Halmashauri ya Rufiji, Tanga halmashauri ya Pangani, Pamoja na Lindi Halmashauri ya Lindi Mjini.