Customer Feedback Centre

Ministry of Health

BMH YAENDELEA KUPANDIKIZA BETRI KWENYE MOYO

Posted on: February 28th, 2024



Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma upasuaji wa kupandikiza betri kwenye moyo kwa watu watatu leo.

Upandikizaji wa betri kwenye moyo ambao kitaalamu inaitwa _pacemakers_ _implantation_ unafanyika kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na kusababisha mapigo ya moyo kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa kwa mtu wa kawaida ambayo ni 60-100 kwa dakika.Wengi wao huwa ni chini ya 40.

Mkuu wa Kliniki ya Moyo wa BMH, Daktari Bingwa wa Moyo, Happiness Kusima, amesema leo kuwa BMH imefikisha upandikizaji kwa watu 18 toka huduma ianzishwe mwaka 2021.

"Jana tumepandika watu watatu (3), leo tutapandikiza watu wawili," amesema Daktari huyo Bingwa wa Moyo.

Dkt Happiness amesema upandikizaji huu unafanyika kwenye kambi ya pamoja kati ya Madaktari Bingwa wa Moyo wa BMH na Daktari Bingwa wa Moyo, George Longopa, kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Kambi hii ya moyo ya pamoja kati ya BMH na JKCI imeanza leo na itakamilika kesho.