Customer Feedback Centre

Ministry of Health

BILION 6.7 ZABORESHA HUDUMA ZA AFYA HANDENI – TANGA.

Posted on: September 30th, 2023

Na. WAF, Handeni -Tanga

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili ameleta kiasi cha shilingi billion 6.7 kwenye Halmashauri ya wilaya ya Handeni ikiwa ni kwa ajili ya Uboreshaji wa Huduma kwenye sekta ya Afya Nchini.


Dkt. Mollel amebainisha hayo wakati akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.


Dkt. Mollel amesema kuwa amepokea maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ni ya kuangalia kwa karibu kwani iko karibu na barabara ya njia panda chalinze kwenda Tanga ambapo kunatokea ajali nyingi hivyo lazima iwe na mahitaji yote muhimu kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya dharura yatakayo tokea wakati wowote.


Aidha ameeleza kuwa mpaka sasa katika hospitali hiyo Huduma zinazopatikana ni Huduma za wagonjwa wa nje, Huduma ya X RAY, Huduma za maabara na Huduma za upasuaji.