Customer Feedback Centre

Ministry of Health

AFYA SPORTS CLUB YANG’ARA MASHINDANO YA SHIMIWI IRINGA

Posted on: October 5th, 2023


Na WAF, Iringa

Timu ya Afya Sport Club imeshiriki mashindano ya michezo ya 37 ya Shirikisho la Michezo la wizara na idara za serikali (SHIMIWI) na kuibuka nafasi ya 2 kwenye mashindano ya riadha mita 3000 na nafasi ya 3 mita 800 huku wakiingia fainali mita 100 na nusu fainali mita 200.


Aidha mashindano hayo yanayohusisha wizara na taasisi za kiserikali yanafanyika mkoani Iringa na yalizinduliwa rasmi na Naibu Waziri mkuu na Waziri wa nishati Dkt. Doto Biteko katika uwanja vya CCM Samora mkoani Iringa.


Aidha timu ya Afya Sports Club imefanikiwa kuingia 16 bora katika mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta Kamba kwa wanaume na wanawake.