SERIKALI, WADAU WAWEKA MIKAKATI YA KUHARAKISHA UTOKOMEZAJI WA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
Posted on: July 31st, 2026NA Cletus Sanga, WAF - Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya afya, maji, usafi wa mazingira na afya ya mazingira katika juhudi za kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs).
Hayo yamesemwa leo Juni 30, 2026 na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Otilia Gowele, wakati wa Jukwaa la WASH-NTD lililofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kutathmini maendeleo yaliyofikiwa, kubaini changamoto na kujadili fursa katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo nchini.
Dkt. Gowele amesema jukwaa hilo ni muhimu katika kuimarisha uratibu na ushirikiano kati ya sekta mbalimbali zinazohusika na afya, maji na usafi wa mazingira, pamoja na kutoa nafasi kwa wadau kujadili mafanikio yaliyopatikana na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazochelewesha kufikiwa kwa malengo ya kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
“Mafanikio ya kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yanategemea ushirikiano madhubuti kati ya sekta mbalimbali. Kupitia jukwaa hili tunaweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kuboresha afya za wananchi na kufikia malengo tuliyojiwekea,” amesema Dkt. Gowele.
Ameongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea kuwekeza katika afua za maji safi, usafi wa mazingira na elimu ya afya kwa jamii, ambazo zimeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuzuia, kudhibiti na hatimaye kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Helen Keller International Tanzania, Dkt. George Kabona, amesema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yanahitaji juhudi za pamoja kutoka Serikalini na kwa wadau wa maendeleo ili kuhakikisha afua za kinga, tiba na udhibiti wake zinawafikia wananchi wote walio katika maeneo hatarishi.
Amesema mafanikio katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo yanategemea uwekezaji endelevu katika huduma za maji safi, usafi wa mazingira, elimu ya afya na upatikanaji wa huduma za matibabu, huku akisisitiza kuwa ushirikiano wa sekta mbalimbali