WIZARA YA AFYA, WHO KUANDAA MPANGO WA KUKABILIANA NA ATHARI ZA JOTO KATIKA MASHINDANO YA AFCON
Posted on: August 3rd, 2026Na WAF-Dar es Salaam
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeanza kuweka mpango mkakati wa kuwawezesha wataalam kutekeleza program ya kuweka mazingira wezeshi ya kukabiliana na athari ya mazingira ya joto kwa wanamichezo, wafanyakazi na washiriki watakaohudhuria mashindano ya AFCON mwaka 2027.
Akifungua kikao cha kupitia miongozo ya utekelezaji wa mpango huo leo Agosti 3, 2026 jijini Dar Es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle amesema Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda zimepata fursa ya kuandaa mashindano hayo makubwa barani barani Afrika ambayo yatashirikisha idadi kubwa ya wageni, hivyo Wizara kwa kushirikiana na WHO imeona ni bora kuanza kujiandaa mapema kuweka mazingira wezeshi ya kukabiliana na athari ya mabadiliko ya mazingira kwa wageni.
Dkt. Gowelle amesema Shirika la Afya Duniani pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) zimekubaliana katika mashindano mbalimbali yanayosimamiwa na FIFA, nchi waandaaji wanatakiwa kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kulinda afya za watoa huduma kwenye sekta ya michezo kupitia programu ya kulinda afya katika sekta ya michezo kupitia mpango wa "Beat the Heat: Flagship Initiative".
Tanzania, Kenya na Uganda zinashirikiana kuandaa mashindano ya mpira wa miguu ya Afrika (AFCON) mwaka 2027, ambapo moja ya afua za kuweka mazingira wezeshi ni kushirikisha makundi ya wafanyakazi watakaotoa huduma kwenye michezo hiyo kupitia zoezi la maigizo ya majaribio ya utayari (Table Top Simulation Exercise (TTX) ili kupima na kuimarisha mifumo ya uratibu, mawasiliano, na mwitikio wa dharura kipindi