KAMATI YASHAURI WADAU KUSHIRIKISHWA KATIKA UENDESHAJI WA MADUKA YA DAWA MUHIMU
Posted on: August 17th, 2026Na Shaban Juma, WAF – Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeishauri Serikali kuwashirikisha wadau katika mchakato wa uboreshaji wa sheria, kanuni na taratibu za uanzishwaji na uendeshaji wa Maduka ya Dawa Muhimu (DLDM) nchini.
Ushauri huo umetolewa leo Agosti 17, 2026, na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Emmanuel Nuwas, wakati Kamati ikipokea taarifa ya Serikali kuhusu usimamizi wa DLDM jijini Dodoma.
Dkt. Nuwas amesema ushirikishwaji wa wadau ni muhimu ili kuhakikisha maboresho ya sheria na kanuni yanaendana na mazingira halisi ya uendeshaji wa DLDM, huku yakilenga kulinda afya za wananchi na kuboresha upatikanaji wa dawa salama.
Kamati imesisitiza umuhimu wa kuongeza udhibiti wa maduka hayo ili kuhakikisha dawa zinatolewa kwa wananchi kwa usalama na kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya. Aidha, imependekeza kuimarishwa kwa usimamizi katika ngazi za chini ili changamoto zinazoweza kujitokeza ziweze kubainika na kuchukuliwa hatua kwa wakati.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, amesema Serikali inaendelea kuimarisha usimamizi na udhibiti wa Maduka ya Dawa Muhimu ili kuhakikisha huduma za dawa zinatolewa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kitaalamu. Amesema usimamizi huo unalenga kuhakikisha dawa zinahifadhiwa na kutolewa kwa usahihi, pamoja na kuhakiki