Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA WATANZANIA KWENYE MAZOEZI, KULINDA AFYA

Posted on: May 4th, 2024



Na WAF - Dar Es Salaam

Waziri Mkuu Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, mapema leo Mei 4,2024 ameongoza mamia ya Watanzania katika mazoezi ili kulinda afya zao na Magonjwa Yasiyoyakuambukiza.

Mazoezi hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ni moja ya afua iliyoa asisiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kama moja ya mikakati yakuondokana na maradhi hayo

“Mnakumbuka programu hii iliyoanzishwa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na yeye mwenyewe kushiriki na kuwahamasisha watanzania kushiriki mazoezi mbalimbali, katika kipindi cha miaka mitatu ya Dkt. Samia moja ya mambo ya kujivunia ni mafanikio kwenye sekta ya michezo.”

Mheshimiwa Majaliwa ametumia wasaa huo kutoa wito kwa Viongozi wa Manispaa ya Kinondoni kufanya maboresho zaidi katika eneo la fukwe za Coco ili liwe safi na livutie watu wa rika mbalimbali.

“Nawapongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri ya ulinzi kwenye eneo hili, Nitoe wito kwenu kuendelea kuimarisha ulinzi ili eneo hili liwe salama kwa watu wa rika na jinsia zote na nyakati zote.”

Awali, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amemshukuru Waziri Mkuu kwa kukubali kushiriki katika mazoezi hayo huku akitoa taarifa ya ongezeko la magonjwa 10 yasiyo ya kuambukiza jambo lililofanya Wizara hiyo kuleta ombi la kuanzisha utaratibu wa mazoezi kila jumamosi.

“Mwaka 2022 kati ya magonjwa 10 yanayowasumbua watanzania moja lililojitokeza ni shinikizo la juu la damu bajeti ya mwaka 2022/2023 likaongezeka na kisukari katika mahlgongwa 10 yanayowasumbua watanzania. Wajibu wa Wizara ya Afya ni kuwakinga Watanzania wasipate magonjwa.”

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albart Chalamila amesema kama Mkoa watajipanga kuhakikisha utaratibu huo wa mazoezi utakuwa endelevu kwa kishirikiana na kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na wadau mbalimbali wa michezo.

Matembezi hayo ya kilomita 10 yalianzia katika fukwe za Coco kupitia daraja la Tanzanite hadi Ocean Road jijini Dar es Salaam.

MWISHO