Wizara Ya Afya

TANZANIA YAONGOZA WITO WA KUIMARISHA UWEKEZAJI KATIKA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Posted on: August 18th, 2026

Na Hassan Kimweri, WAF - Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema nchi za Afrika zinapaswa kuongeza uwekezaji wa uhakika na ubunifu katika afya ya mama, mtoto na huduma za afya ya msingi ili kuimarisha usalama na kujitegemea kwa afya barani Afrika.

Waziri wa Afya Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo, Agosti 18, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akihutubia Mkutano wa Nne wa Kamati ya Mawaziri ya Uendeshaji wa Kikanda ya Afrika Mashariki (ReSCO), akiwa Mwenyekiti wa mkutano huo.

"Afrika inapaswa kuchukua jukumu la afya yake yenyewe, kwa kuwa afya ya mama na mtoto ni kipimo muhimu cha utendaji wa mifumo ya afya na maendeleo ya mataifa, mama na mtoto wanapokuwa salama, familia huwa imara, jamii huwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto na taifa huwa salama zaidi," amesema Waziri Mchengerwa

Aidha, Waziri Mhe. Mchengerwa amesema hali ya vifo vya mama na watoto barani Afrika bado ni changamoto, ambapo takwimu za Umoja wa Mataifa za mwaka 2025 zinaonyesha kiwango cha vifo vya uzazi kuwa vifo 454 kwa kila vizazi hai 100,000, huku vifo vya watoto chini ya miaka mitano vikifikia 71 kwa kila vizazi hai 1,000.

Katika hatua nyingine, Waziri Mhe. Mchengerwa amesema Afrika Mashariki inakabiliwa na vitisho vya kiafya vinavyovuka mipaka, ikiwemo milipuko ya Ebola, kipindupindu na mpox, pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi na migogoro ya kibinadamu.

"Nchi zetu za Afrika hazipaswi kusubiri dharura itokee ndipo zianze kushirikiana, bali ziimarishe ufuatiliaji wa magonjwa mipakani, maandalizi ya pamoja, maabara na vituo vya dharura za afya ya umma," amesema Waziri Mhe. Mchengerwa

Akizungumzia Tanzania, Mhe. Mchengerwa amesema uwekezaji unaoendelea katika sekta ya afya umeongeza upatikanaji wa huduma, ambapo kati ya asilimia 80 ya Watanzania wanaweza kupata huduma za afya ndani ya kilomita tano kutoka wanapoishi.

"Serikali itaendelea kuimarisha uwezo wa kitaifa na kikanda wa kujiandaa na kukabiliana na milipuko ya magonjwa, akisisitiza kuwa nchi za Afrika Mashariki zinapaswa kuimarisha ushirikiano na uwekezaji katika afya ya msingi, mama na mtoto ili kujenga mifumo ya afy