SERIKALI KUENDELEA KUWEKEZA KINGA KUKABILI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
Posted on: February 1st, 2026Na WAF, Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarisha uwekezaji kwenye kinga ili kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, ikiwa ni mkakati wa kupunguza mzigo wa maradhi yanayozuilika na kuboresha afya ya jamii.
Akizungumza na wanahabari Mkoani Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani Januari 30, 2026, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa (MB), amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza jitihada na rasilimali za ndani ili kuhakikisha mapambano dhidi ya magonjwa hayo yanafanyika kwa uendelevu.
“Serikali imeamua kuwekeza zaidi kwenye kinga kwa kutumia rasilimali zake yenyewe ili kulinda afya ya mwananchi na kupunguza gharama za matibabu,” amesema Mhe. Mchengerwa
Amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2024/25 hadi 2025/26, Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 6.9 za fedha za ndani kwa ajili ya utekelezaji wa afua za kudhibiti na kutokomeza magonjwa hayo, ikiwemo ugawaji wa kingatiba, huduma za upasuaji na uimarishaji wa mifumo ya taarifa za afya.
Mhe . Mchengerwa amesisitiza kuwa uwekezaji huo ni hatua muhimu ya kupunguza utegemezi wa wafadhili.
Aidha amesema kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, mwaka 2025 zaidi ya watu milioni 4.3 walipatiwa kingatiba dhidi ya ugonjwa wa Usubi katika Halmashauri 21, sawa na asilimia 99 ya walengwa. Aidha, watoto zaidi ya milioni 2.4 walipatiwa dawa za Minyoo ya Tumbo sawa na asilimia 94 ya lengo, huku watoto zaidi ya milioni 1.7 wakimeza kingatiba za Kichocho, sawa na asilimia 96 ya walengwa.
Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana, Mhe. Mchengerwa amesema kuwa Halmashauri 114 kati ya 119 zilizokuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Matende na Mabusha zimefanikiwa kupunguza maambukizi na kusimamisha ugawaji wa kingatiba katika ngazi ya jamii.
“Mafanikio haya yanaonesha wazi kuwa kinga inalipa na ina matokeo chanya kwa afya ya jamii,” amesema.
Amesema pia Serikali imeanza rasmi mageuzi ya matumizi ya teknolojia kwa kuanzisha mfumo wa kidijitali wa CMIS–DHIS2 kwa ajili ya kuripoti takwimu za magonjwa hayo, am