PROF. ABEL MAKUBI MKURUGENZI MPYA HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA
Posted on: June 4th, 2024
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo mkoani Dodoma.
Kabla ya uteuzi huu Prof. Makubi alikuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubongo Muhimbili
(MOI).
Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dkt. Alphonce Biola Chandika ambaye amemaliza muda wake.