MAFUNZO KWA VITENDO KUONGEZA TIJA UTOAJI WA HUDUMA
Posted on: January 31st, 2026Na WAF, Rufiji
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Rufiji, Dkt. Sajidu Ismail, amesema zoezi la utoaji wa mafunzo kwa vitendo kwa wahudumu wa afya kwa huduma za Wagonjwa Mahututi (ICU) na huduma za Dharura (EMD) kwa mkoa wa Pwani, litaongeza tija na kuimarisha ujuzi wa wataalamu wa afya.
Dkt. Ismail ameyasema hayo leo Januari 29, 2026 katika Halmashauri ya Mji Rufiji, Mkoa wa Pwani, kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Wilaya.
Amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI wamewezesha upatikanaji wa Wataalamu wa afya wanaotoa mafunzo hayo kwa muda wa siku nne katika kila Wilaya ya Mkoa huo, ikiwemo Rufiji, Kibiti, Kisarawe na Bagamoyo. Amesisitiza kuwa mafunzo hayo yataimarisha zaidi utoaji wa huduma katika vituo vya afya vya wilaya hizo.
Dkt. Ismail ameongeza kuwa Halmashauri ya Mji Rufiji inasimamia jumla ya vituo vya afya 37, hivyo kupitia mafunzo hayo, watahakikisha Ujuzi unaopatikana unasambazwa pia kwa Vituo vya jirani ili kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi wa Wilaya ya Rufiji.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ikwiriri, Dkt. Nassibu Abdallah Mdoka, amesema ujio wa madaktari bingwa katika kituo hicho umewaongezea uwezo watumishi katika matumizi ya vifaa tiba vya kisasa ambavyo awali havikutumika ipasavyo. Amesema hali hiyo itasaidia kupunguza Rufaa za wagonjwa kwenda hospitali za nje ya Wilaya.
Dkt. Mdoka ameishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga jengo la kisasa la huduma za dharura katika kituo hicho pamoja na kuleta Madaktari bingwa wanaoendelea kuwajengea uwezo watumishi, jambo litakalosaidia kupunguza Rufaa na kuongeza matumizi sahihi ya mashine za kisasa zilizokuwepo.
Naye Daktari Kiongozi wa Kitengo cha Dharura, Dkt. Advesta Konga, amesema wamefurahishwa na ujio wa madaktari bingwa waliotoa mafunzo elekezi kuhusu huduma za dharura na uangalizi wa wagonjwa mahututi. Amesema mafunzo hayo yatachangia kupunguza Rufaa zisizo za lazima, vifo vinavyoweza kuzuilika na kuongeza ufanisi wa matumizi ya vifaa tiba, ikiwemo mashine ya kusaidia kupumua (ventilator).
Madaktari bingwa kutoka Wizara ya Afya wanaoratibu mafunzo hayo wamesema wanaamini kuwa wahudumu wa