Wizara Ya Afya

DKT. GRACE MAGEMBE AHIMIZA WANANCHI KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE, ASISITIZA KINGA NI BORA KULIKO TIBA

Posted on: July 8th, 2026

Na Aisha Swahibu, WAF - Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kujiandikisha na kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote, huku akieleza kuwa mfumo huo utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wakati, kupunguza gharama za matibabu kwa familia na kuimarisha ustawi wa afya za Watanzania.

Dkt. Magembe ameyasema hayo Leo Julai 8, 2026 wakati akitembelea mabanda ya Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) Dar es Salaam. Mabanda yaliyotembelewa ni MSD, TMDA, TIRA, MNH, ORCI, JKCI, NHIF, MOI, Hospitali binafsi ya Epiphany na Hospitali ya Police Kilwaroad.

Dkt. Magembe watumishi wa afya wanaotoa huduma katika mabanda ya Sabasaba kuhakikisha wanatoa elimu sahihi kwa wananchi kama ilivyo Kampeni ya zijue namba zako iliyozinduliwa na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujua viashiria vya magonjwa kwa kupima urefu, uzito, shinikizo la damu, kiwango cha sukari kwenye damu, mapigo ya moyo, kuwahamasisha wananchi kuepuka matumizi makubwa ya chumvi, sukari, mafuta ya kula, pombe , uvutaji wa sigara na kutofanya mazoezi.

“Tukiweza kuwahamasisha wananchi kufanya uchunguzi wa Afya zao mara kwa mara, wataweza kugundua magonjwa mapema kabla hayajafikia kiwango cha juu”, amesema Dkt. Magembe

Katika hatua nyingine, Dkt. Magembe ameitaka Bohari ya Dawa (MSD) kuimarisha kitengo cha Ubunifu na tafiti kwa kuweka dawati la kuwasikiliza na kuwasaidia vijana wa kitanzania ambao kwa sasa wamekuja na ubunifu katika matumizi ya akili unde na utengenezaji wa vifaa tiba, kwa lengo la kukuza vipaji vya ndani na kutengeneza ajira kwa vijana.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa wananchi kupima afya zao mara kwa mara ili kubaini changamoto za kiafya mapema na kupata matibabu kwa wakati kabla magonjwa hayajawa makubwa.

Vilevile, Dkt. Magembe amesisitiza kuendelea kutolewa kwa elimu kuhusu kampeni ya “Vaa Helmeti, Ubongo Hauna Spea”, akibainisha kuwa ajali nyingi za barabarani zinazohusisha waendesha bodaboda husababish