Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

BIMA YA AFYA KUTOA FURSA YA MWANANCHI KUTIBIWA HOSPITALI YOYOTE ANAYOITAKA- PROF. MAKUBI

Posted on: October 12th, 2022



Na WAF - DSM

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa, Bima ya Afya kwa wote itatoa fursa kwa Mtanzania mwenye hali yoyote kwenda kupata matibabu katika hospitali yoyote zikiwemo hospitali za kitaifa kama Muhimbili na nyingine za kibingwa.

Prof. Makubi amesema hayo, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Mkoa ya Amana, ambapo alipata fursa ya kuongea Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Amana, Mwananyamala, Temeke, Tumbi, Mbagala Rangitatu, Kigamboni walioongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na pamoja na tkamati za usimamizi za afya za Halmashauri.

"Kumbukeni Bima ya Afya itakapopitishwa Mgonjwa atakuwa na haki ya kutibiwa hospitali yoyote anayoitaka, yaweza kuwa hospitali ya binafsi au ya Serikali, sasa niwakumbushe kujipanga vizuri katika kutoa huduma bora na kutatua kero za wananchi ikiwemo kukaa muda mrefu, matumizi ya lugha nzuri na misongamano isiyo ya lazima." Amesema Prof. Makubi.

Amesema, wananchi wana haki yakupatiwa huduma bora, hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali imewekeza katika upatikanaji wa dawa, miundombinu bora, vifaa tiba pamoja na ongezeko la Watumishi katika maeneo ya kutolea huduma za afya nchini.

Serikali inaendelea kuelekeza kuweka kitengo cha huduma kwa mteja katika maeneo yote yakutolea huduma za afya kitachosaidia kupata mrejesho kutoka kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa, huku akisisitiza vitengo hivyo vitapunguzia usumbufu wananchi wanaofika kupata huduma. Amesisitiza Prof. Makubi.

Sambamba na hilo, ameelekeza uongozi wa Hospitali kutoa mafunzo ya huduma kwa mteja ikiwemo matumizi ya lugha nzuri na zenye staha kwa walinzi wa usalama wanaochaguliwa kwenda katika vituo vya kutolea huduma ili kuondoa malalamiko yanayoweza kuzuilika kutoka kwa wananchi.

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema, Mkoa wa Dar es Salaam umejipanga vizuri kuelekea kuanza kutekeleza matumizi ya Bima ya Afya kwa wote, kwani hali ya upatikanaji wa dawa zilizo katika mwongozo (STG) imefika zaidi ya asilimia 90, huku ujenzi na uboreshaji wa huduma ukiendelea...