MHE. MCHENGERWA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO SAME, MWANGA
Posted on: July 23rd, 2026Na John Mapepele, WAF - Kilimanjaro
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Watendaji wa Serikali kuwa wabunifu na kuzishirikisha taasisi na wadau mbalimbali katika kuwaletea watanzania maendeleo.
Mheshimiwa Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo wakati akiwa katika siku yake ya kwanza kwenye ziara ya kikazi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali katika kipindi hiki katika wilaya ya Same na Mwanga.
Akikagua mradi wa ujenzi wa madarasa kwenye shule ya Msingi ya Lungwana katika wilaya ya Same, waziri Mchengerwa amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kuzishirikisha taasisi za Wakala wa Misitu nchini TFS ili isaidie kutoa miti kwa ajili ya kutengenezea madawati ya madarasa yaliyo kamilika.
Amesema hakuna maana yoyote kama madarasa hayo hatakawekwa madawati ili hali tayari yameshakamilika na amesisitiza kuwa taasisi kama TFS na TANAPA wanayo mafungu ya kurejesha kwa jamii zinazozunguka maeneo hayo kwa kuwa jamii hiyo inashiriki kwenye uhifadhi.
Amewasihi kama hakuna magogo yaliyovunwa kimakosa ambayo yamekusanywa, basi serikali ya kijiji iombe kibali ili mkavune misitu huku akiendelea kuhoji kuwa hakuna faida yoyote ya kuwa na misitu wakati watoto wanakaa chini.
"Ndugu zangu ni muhimu kujiongeza siyo kila kitu kutegemea Mheshimiwa Rais aweze kufanya hata hivi vidogo vidogo, Rais tayari ametoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi hii". amefafanua
Kwa mujibu wa taarifa ya mkoa iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe.Nurdin Babu katika kipindi cha miaka mitano tayari Serikali imeshatoa shilingi trioni 1.5 kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye mkoa huu.
Pia, akikagua hospitali ya Wilaya ya Mwanga ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuendelea kuwa wabunifu katika kuboresha huduma badala ya kungojea fedha kutoka Serikalini.
Amesema wakati umefika kwa viongozi kujitathimini kama wanastahili kuwepo kwenye nafasi hizo bila kuzitendea haki huku akisisitiza kuwa Tanzania ina watu wengi wenye uwezo wa kufanya kazi hivyo watendaji na wataalam waliopata bahati ya kuwa kwenye nafasi hizo hawana budi kuzite