Wizara Ya Afya

KYERWA YAUPOKEA MKAKATI KUKABILI EBOLA NA KUAHIDI KUUENDELEZA

Posted on: July 24th, 2026

Na Mvuda Jaffer, WAF-Kyerwa

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Bi. Zaituni A. Msofe, amepongeza na kuahidi kuupokea na kuuendeleza mpango wa serikali wa utayari kwa wananchi kukabiliana na changamoto ya magonjwa ya mlipuko kama Ebola endapo yakitokea hasa ikizingatiwa kuwa eneo hilo lipo jirani na nchi zinazotajwa kuwa na mlipuko wa Ugonjwa huo.

amesema hayo leo Julai 24, 2026 wakati wa mafunzo kwa viongozi wa jamii kuhusu utayari wa kukabiliana na tishio la magonjwa ya mlipuko, mafunzo yanafanywa kwa ushirikiano wa Serikali na Mdau wa Maendeleo CIHEB Tanzania chini ya Mradi wa Usalama wa Afya Duniani wilayani humo.

Bi.Msofe amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha wananchi wanalindwa dhidi ya majanga ya afya ya umma kwa kujenga jamii yenye uelewa na uwezo wa kuchukua hatua sahihi wakati wote.

Aidha,ameomba Serikali na Wadau kuendelea kuwekeza katika utoaji wa elimu kwa wananchi wa maeneo ya mipakani kwani jamii ndiyo nguzo kuu ya mafanikio ya hatua zote za kudhibiti magonjwa ya mlipuko. Wananchi wakipata elimu sahihi watatambua dalili mapema, watatoa taarifa kwa wakati na kushirikiana na wataalamu wa afya katika kuzuia magonjwa haya yasienee.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bw.Marco J.John amesema ujio wa timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya umeongeza nguvu katika juhudi za halmashauri za kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa kuwajengea uwezo viongozi wa jamii watakaokuwa kiungo muhimu kati ya sekta ya afya na wananchi.

“Elimu inayotolewa itaongeza ushiriki wa jamii katika shughuli za ufuatiliaji wa magonjwa, utoaji wa taarifa kwa wakati na utekelezaji wa afua mbalimbali za afya ya umma, huku akisisitiza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Wizara ya Afya, mamlaka za serikali za mitaa na wananchi ni msingi wa kujenga mfumo imara wa utayari na mwitikio dhidi ya magonjwa ya mlipuko.”amesema Bw.John

Washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza Wizara ya Afya kwa kuwafikishia elimu hiyo na Pia wamependekeza kuimarishwa kwa kampeni za uelimishaji kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara, kuongeza vifaa