Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WATALAAM WA OPTOMETRIA (UREKEBISHAJI UPEO WA MACHO KUONA) WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI WAKATI WA UTOAJI WA HUDUMA

Posted on: November 28th, 2023

Na WAF – Dodoma

Hayo yamesemwa 23 Novemba na Msajili wa Baraza la Optometria Bw. Sebastiano G. Millanzi katika kikao cha uboreshaji wa huduma za macho Mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, kilichokutanisha wataalam wa Optometria pamoja na wamiliki wa vituo vya Optometia vikiwemo; Kliniki za Optometria, vituo vya usambazaji wa vifaa tiba vya macho (Miwani, fremu na lenzi), Maabara za Optometia na Viwanda vya Optometria.

“Lengo kuu la kikao hiki ni kuwakumbusha watalaam na wamiliki wa vituo vya Optometria kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo iliyopo wakiwa katika maeneo yao ya kazi hasa uzingatiwaji wa maadili wakati wa utoaji wa huduma kwa jamii” amesema Bw. Sebastiano Millanzi

“Aidha, kumekuwako na watoa huduma ambao hawana utalaam wowote katika taaluma ya Optometria wanaojifanya kama wataalam, tunawataka watu wa aina hiyo kuacha mara moja kuwalaghai watanzania. Lengo likiwa ni kulinda afya ya macho kwa jamii", amesema Bw. Sebastiano G Millanzi

Katika hili, Bw. Sebastiano G. Millanzi amewaasa watanzania kuachana na tabia ya kujinunulia miwani barabarani au katika vituo visivyoeleweka pasipo kupimwa au pasipo ushauri wa mtaalam wa macho; hivyo jamii imeshauriwa kwenda kupata huduma za macho katika vituo vinavyotambulika Kisheria kama vile Hospitali, vituo vya afya vilivyosajiliwa na Serikali ndipo uanze kutumia aina fulani ya miwani.

Pia, Bw. Sebastiano G. Millanzi amewasititiza wataalam kutoa rufaa kwa wagonjwa wanaoenda kupata huduma katika Kliniki zote za Optometria na vituo vingine ili waweze kupata uchunguzi wa kina wa macho au mwili kwa ujumla uweze kufanyika (Comprehesive Eye Checkup).

“Kwa lengo zima la kuzuia changamoto ya upofu unaoweza kuzuilika, tunawasisitiza watalaam wa Optometria kutoa rufaa katika hatua za awali kwa wagonjwa ambapo changamoto nyingine zinaweza kubainika na kupatiwa matibabu"

Aidha Bw. Sebastiano Milanzi amewataka watalaam wa Optometria kuhuisha leseni zao mara moja.