Customer Feedback Centre

Ministry of Health

TUENDELEE KUWEKEZA KWENYE UBUNIFU WA TEKNOLOJIA YA AFYA

Posted on: April 10th, 2025

Na WAF, Zanzibar


Serikali itaendelea kuwekeza nguvu zaidi  katika ubunifu na ugunduzi wa teknolojia zinazolenga kuimarisha sekta ya afya nchini ili kupunguza utegemezi wa teknolojia kutoka nje na gharama kubwa za ununuzi wake.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo Aprili 10, 2025 wakati wa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Sayansi ya Moyo (The 3rd Heart Team Africa 

Cardiotan 2025) uliofanyika Zanzibar, Dkt. Mollel amesema kuwa maendeleo ya sekta ya afya hayawezi kufikiwa bila kuwawezesha wabunifu wa ndani kushiriki kikamilifu katika kutatua changamoto za kiafya.


"Ni muhimu kuwekeza kwenye ubunifu wa teknolojia ya afya kama njia ya kupunguza utegemezi wa teknolojia kutoka nje na gharama kubwa za ununuzi wake, tukiwawezesha wabunifu wa ndani, tutakuwa tunatafuta suluhisho endelevu kwa changamoto zetu kwa kutumia rasilimali na uelewa wa mazingira yetu," amesema Dkt. Mollel.


Dkt. Mollel amehimiza taasisi za utafiti, vyuo vikuu, na sekta binafsi kushirikiana katika kuendeleza teknolojia zitakazorahisisha utoaji wa huduma bora za afya kwa Watanzania.


Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na umewakutanisha wataalam wa afya ya moyo kutoka ndani na nje ya Afrika kujadili mbinu bora za uchunguzi, matibabu, na upasuaji wa magonjwa ya moyo.