Customer Feedback Centre

Ministry of Health

SERIKALI KUONGEZA UZALISHAJI WA NDANI WA BIDHAA ZA AFYA.

Posted on: October 24th, 2023

Na WAF - NJOMBE


Serikali kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kuongeza uzalishaji wa bidhaa za Afya Nchini ikiwemo Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba kwa kupitia viwanda vya ndani vinavyoendelea kuzalisha bidhaa hizo ikiwemo kiwanda cha mipira ya mikono (gloves). 


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Oktoba 24, 2033 alipotembelea kiwanda cha kuzalisha mipira ya mikono (gloves) kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kilichopo Idofi katika Wilaya ya Makambako Mkoani Njombe. 


“Tumedhamiria kuongeza uzalishaji wa ndani wa bidhaa za Afya ikiwemo Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba kwa kuwa sasa hivi tunaagiza vifaa hivyo nje ya nchi kwa 85% ikiwemo Dawa, Gloves, Vitendanishi pamoja na vifaa vingine vya Afya”. Amesema Waziri Ummy.


Amesema, unaponunua nje ya nchi bidhaa za Afya kuna changamoto nyingi ikiwemo kuchukua mda mrefu zaidi ya miezi Tisa hadi dawa kufika nchini ambapo inapelekea kuwa na kilio cha uhaba wa dawa na vifaa tiba. 


Pia, amesema changamoto nyingine ni kutumia fedha za kigeni kuagiza bidhaa hizo ambapo huoelekea kupoteza fedha nyingi, uwepo na bidhaa duni (zisizofaa) kuingia nchini. 


Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa lengo la Serikali kupitia Wizara ya Afya ni kufikia asilimia 50 ya bidhaa zote za Afya ziwe zinanunuliwa ndani ya nchi kupitia Bohari ya Dawa (MSD).


“Tumejiwekea malengo hadi kufikia 2030 tunataka kufika asilimia 50 ili tuweze kuokoa fedha zisipotee nje ya nchi na kupunguza changamoto nyingine na tunaenda vizuri ambapo kwa sasa uzalishaji wa ndani ni asilimia 20”. Amesema Waziri Ummy 


Wakati akiendelea kuzungumza Waziri Ummy amesema Tanzania kuna viwanda takriban 30 vya dawa na vifaa tiba ambapo viwanda 11 vinafanya kazi ikiwe kiwanda hicho cha mipira ya mikono chenye uwezo wa kuzalisha mipira zaidi ya Mil. 80 kwa mwaka. 


“Lakini pia tuna viwanda vingine viwili vya maji tiba (Drip) vyenye uwezo wa kuzalisha chupa Mil. 90 kwa Mwaka ambapo mahitaji ya yetu ni chupa Mil. 24 kwa 26”. Amesema Waziri Ummy