Customer Feedback Centre

Ministry of Health

RC KATAVI, WANANCHI JITOKEZENI KWA WINGI KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA

Posted on: September 30th, 2025

Na WAF, Katavi

Wananchi wa Halmashauri tano (5) za mkoa wa Katavi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma za matibabu ya kibingwa zinazoanza kutolewa leo na Madkatari Bingwa wa Huduma za Mkoba mkoani humo.

Madaktari Bingwa wa Rais Samia wanaanza kutoa huduma leo Septemba 29, hadi Oktoba 3, 2025 mkoani katavi lengo likiwa ni kutoa tiba za kibingwa karibu na wananchi kutoka Halmashauri zote tano (5) za mkoa wa Katavi.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Bi. Mwanavua Mrindoko ametoa wito kwa wakazi wote wenye changamoto za kiafya kujitokeza kupata huduma hiyo akisema hii ni ushuhuda mwingine wa kiutu kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kiongozi huyo wa mkoa amezitaja faida za uwepo wa huduma za Madaktari wa Rais Dkt. Samia kuwa ni pamoja na kutoa huduma hizo karibu kabisa na jamii, kujenga uwezo kwa watoa huduma wenyeji wa halmashauri ikiwemo kupunguza gharama za kupata huduma hizo nje ya mkoa wake.

Huduma zitakazotolewa ni huduma za kibingwa za magonjwa ya wanawake na ukunga, kinywa na meno, watoto wachanga, mkojo, usingizi pamoja na magonjwa ya ndani.

Mkoa wa Katavi umepokea Madaktari Bingwa 30 na wauguzi Bingwa watano (5) ambao watakuwa katika kambi tano(5) kwa kila Halmashauri.